Tanzania Tanzania Nakupenda kwa moyo wote Nchi yangu Tanzania Jina lako ni tamu sana Nilalapo nakuota wewe Niamkapo ni heri mama wee Tanzania Tanzania Nakupenda kwa moyo wote
Tanzania Tanzania Ninapokwenda safarini Kutazama maajabu Biashara nayo makazi Sitaweza kusahau mimi Mambo mema ya kwetu kabisa Tanzania Tanzania Nakupenda kwa moyo wote
Tanzani Tanzania Watu wako ni wema sana Nchi nyingi za kuota Nuru yako hakuna tena Na wageni wa kukimbilia Ngome yako imara kweli wee Tanzania Tanzania Heri yako kwa mataifa
Tanzania Tanzania Karibu wasio na kwao Wenye shida na taabu Hukimbizwa na walo wezi Tanzania yawakaribisha Tuungane kiume chema wee Tanzania Tanzania Mola awe na we daima.